Trending

Young Africans Waifuata Dodoma Jiji.

 

Klabu ya soka ya Young Africans imewafuata Dodoma Jiji Fc katika mchezo wa NBC Premier League utakaochezwa katika uwanja wa Airtel Singida, tarehe 13 May, 2026 kuanzia saa Kumi na robo jioni.

Mlinda lango wa Young Africans, Hussen Masalanga amewaomba shabiki na wapenzi wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu yao.

“Kwa niaba ya Wachezaji wenzangu tumejiandaa vizuri na mchezo wa kesho na kila mmoja wetu anajua umuhimu wake. Kwa sasa lengo letu ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo. 

"Mashabiki wetu wamekuwa msaada mkubwa sana msimu mzima. Tunahitaji sauti yao, nguvu yao na sapoti yao katika kila mchezo. Tunawaomba wajitokeze kwa wingi kesho ili kutupa nguvu ya kupambana na kupata ushindi.”  amesema  Masalanga .

 

🎮 Dodoma Jiji vs Young Africans

📅 13 May, 2026

⏱️ 16:15 pm

🏟️ Airtel Singida

 

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form