Trending

USAJILI: Zunon Kipré Kutoka MC Alger, arejea Azam FC


Klabu ya Azam FC imefikia makubaliano na mabingwa wa Algeria, MC Alger, ya kumrejesha mshambuliaji raia wa Ivory Coast, Zunon Kipré Emmanuel Junior, kuelekea msimu wa 2026/27.

MC Alger imethibitisha kupitia ukurasa wake rasmi wa Facebook kuwa Kipré hataendelea kuwa sehemu ya kikosi hicho msimu ujao, baada ya makubaliano kufikiwa na Azam FC kuhusu uhamisho wake.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo, makubaliano hayo pia yanajumuisha kipengele kinachoiruhusu MC Alger kupata asilimia 30 ya ada ya uhamisho endapo Azam FC itamuuza mchezaji huyo kwa klabu nyingine siku zijazo.

Kipré alijiunga na MC Alger mwaka 2024 kwa mkataba wa miaka mitatu, lakini ameondoka baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa misimu miwili. Katika kipindi hicho, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alifunga mabao matano na kutoa pasi sita za mabao.

Licha ya takwimu hizo, Kipré ameondoka akiwa amechangia mafanikio ya MC Alger kwa kutwaa mataji matatu makubwa, ambayo ni mataji mawili ya Ligi Kuu ya Algeria, ikiwemo taji la kihistoria la 10 la klabu hiyo, pamoja na Kombe la Super Cup la Algeria.

Sasa mshambuliaji huyo anarejea Azam FC akiwa na lengo la kuimarisha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kuelekea msimu mpya wa mashindano ya ndani na kimataifa.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form