Trending

TETESI: Simba, Yanga vitani kuinasa saini ya Winga wa Shekhukhune United

Ushindani kati ya Simba SC na Yanga SC umehamia rasmi kwenye dirisha la usajili, baada ya klabu hizo mbili kuingia katika mbio za kuwania saini ya winga wa Shekhukhune United ya Afrika Kusini, Keletso Makgalwa, kuelekea msimu wa 2026/27.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Afrika Kusini, vigogo hao wa soka Tanzania wameanza kufanya mawasiliano na nyota huyo, kila mmoja akilenga kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

Makgalwa, ambaye ameonnesha kiwango bora akiwa na Shekhukhune United, anatajwa kuwa yupo tayari kutafuta changamoto mpya, hali iliyovutia klabu kadhaa, zikiwemo Simba na Yanga.

Vyanzo vinaeleza kuwa mazungumzo bado yanaendelea kati ya pande husika, huku kila klabu ikijaribu kufikia makubaliano yatakayowezesha kukamilisha usajili huo kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Iwapo mmoja wa vigogo hao atafanikiwa kupata saini ya Makgalwa, usajili huo unatarajiwa kuongeza ushindani mkubwa ndani ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/27, kutokana na uzoefu na ubora wa winga huyo aliouonesha katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

Hata hivyo, hadi sasa hakuna klabu iliyothibitisha rasmi kufikia makubaliano na mchezaji huyo, huku mashabiki wa Simba na Yanga wakisubiri kuona ni upande gani utakaoshinda vita hiyo ya usajili.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form