Trending

Young Africans (Yanga) yaangukia jino la TPLB, Dabi yawapokonya Shilingi Milioni 30.


Klabu ya soka ya Young Africans (Yanga) imejikuta katika jino la Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) baada ya kutozwa faini ya TSh milioni 30 kufuatia ukiukwaji wa taratibu za mchezo katika Dabi ya Kariakoo.

Yanga wamepata adhabu hiyo mara baada ya kukwepa kutumia chumba rasmi cha kubadilishia nguo katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo Stadium na badala yake kutumia nyumba iliyopo nje ya uwanja huo upande wa pili.

Tukio hilo lilitokea Mei 3, 2026 wakati wa mchezo wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba SC uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Katika adhabu nyingine, Meneja wa Yanga, Walter Harson, amefungiwa michezo mitatu pamoja na kutozwa faini ya Sh milioni moja kwa kosa la kumsukuma kiungo wa Simba SC, Clatous Chama, wakati wa mchezo huo.

Maamuzi hayo yalifanywa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa TPLB katika kikao chake kilichofanyika Mei 9, 2026.

Mbali na hilo, Yanga pia imepewa onyo kali baada ya kuchelewa kuwasili uwanjani kwa mchezo huo, ambapo ilifika saa 10:35 alasiri badala ya saa 10:30 alasiri kama kanuni za ligi zinavyoelekeza. 



Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form