Trending

Simba SC Yatambia Taji la CRDB Federation Cup Jangwani Baada ya Parade ya Mabingwa

Baada ya kutwaa ubingwa wa CRDB Federation Cup kwa kuichapa Azam FC bao 1-0 katika fainali iliyochezwa Julai 4, 2026, Simba SC leo imefanya parade ya kusherehekea ubingwa huo huku ikiwatambia watani wao wa jadi, Yanga SC.

Parade hiyo ilianza majira ya saa 4:00 asubuhi na kupita katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam. Msafara wa mabingwa hao ulifika hadi eneo la Jangwani, yalipo makao makuu ya Yanga SC, ambapo ulipokelewa kwa shamrashamra kubwa kutoka kwa mashabiki wa Simba.

Baadhi ya mashabiki wa Simba walionekana wakicheza na kuimba nyimbo za kushangilia ubingwa huo, huku wengine wakielekea katika Uwanja wa Kaunda kuendelea na sherehe za ushindi.

Katika parade hiyo, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, aliwaonesha mashabiki mataji mawili yaliyotwaliwa na klabu hiyo, likiwemo taji la CRDB Federation Cup pamoja na Kombe la Muungano, ambalo Simba ililitwaa baada ya kuifunga Yanga SC bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali.

Parade hiyo ilihitimisha rasmi shamrashamra za Simba SC kufuatia mafanikio ya kutwaa mataji hayo mawili, huku maelfu ya mashabiki wakijitokeza kusherehekea pamoja na timu yao katika maeneo mbalimbali ya jiji.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form