Trending

Yanga yaachia nyuzi. Yapokea kipigo kutoka kwa Dodoma Jiji Fc.

Klabu ya soka ya Young Africans 'Yanga' imeangukia pua baada ya kupokea kipigo cha bao 3 kwa 2 ugenini dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Airtel Singida.

Yanga walianza kupata bao la mapema katika dakika ya 2'' lililofungwa na Allan Okello na baadaye Dodoma Jiji kusawazisha katika dakika ya 29 baada ya mlinzi wa Yanga; Bakari Mwamnyeto kujifunga.

Yanga waliongeza bao la pili lililofungwa na Allan Okello katika dakika ya 41'', lakini katika dakika za jioni 90''; Dodoma Jiji walisawazisha kupitia kwa  Mwani Kibuta.

Yanga walijikuta wanaacha alama alama 3 kwa kufungwa bao la 3 katika dakika ya 90+6 lililofungwa na Wazir Jr.

Yanga imesalia na alama 54 kwenye msimamo wa ligi wakiwa mbele kwa alama 5 na wakiwa mbele kwa mchezo mmoja dhidi ya wapinzani wao wakubwa; Simba Sc ambao wao watacheza kesho. Simba wana alama 49 hadi sasa.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form